Wafanyibiashara Katika Eneo La Mti Moja Mjini Eldoret Wameamkia Tukio La Kuvunja Moyo Baada Ya Maeneo Yao Ya Kufanyia Biashara Kubomolewa Usiku Wa Kuamkia Leo. Wakiongea Na Wanahabari Wafanyibiashara Hao Wameilaumu Serikali Ya Kaunti Ya Uasingishu Kwa Ubomozi Huo Huku Wakidai Wana Hati Miliki Ya Kuonyesha Umiliki Wa Shamba Hilo. Wamepuuzilia Mbali Madai Ya Serikali Ya Kaunti Kuwa Nyumba Za Biashara Zao Zilikuwa Zimejengwa Mahali Pasipostahili Huku Wakidai Ubomozi Huo Ulifanywa Kwa Nia Mbaya. Hata Hivyo Mwakilishi Wadi Wa Kiplombe Rammadhan Ali Amekashifu Tukio Hilo Akiitaka Idara Husika Kuwa Na Utu.
Comments