Tamko la Rais wa Egypt, Abdel Fattah el-Sisi, kwamba nchi yake iko tayari kuisaidia Saudi Arabia katika kukabiliana na mashambulizi ya wapiganaji wa Kihouthi nchini Yemen limefungua ukurasa mpya wa mjadala kuhusu usalama wa Mashariki ya Kati na Bahari Nyekundu.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo mbalimbali vya habari duniani Misri imetangaza utayari wa kutoa msaada unaohitajika kwa Saudi Arabia, huku rais wa nchi hiyo Abdel Fattah el-Sisi akiomba Bunge liidhinishe msaada wa kijeshi ikiwa Riyadh itaomba rasmi. Hata hivyo, tamko la utayari wa kusaidia halimaanishi kwamba Egypt tayari imetuma vikosi kupigana nchini Yemen.
Swali kubwa sasa linabaki kuwa?: iwapo Misri itaingia moja kwa moja katika mzozo huo, athari zipi zinaweza kujitokeza kwa nchi hizo, Yemen na uchumi wa dunia?