Skip to playerSkip to main content
  • 2 days ago
Hebu fikiria unaishi katika moja ya nchi tajiri zaidi duniani, una kazi, lakini kila siku gharama za chakula, mafuta, umeme na nyumba zinazidi kupanda!
Hali hii ndiyo inayoongeza hasira za wananchi katika baadhi ya nchi za Ulaya, huku Ufaransa ikiwa miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na maandamano makubwa zaidi na ghasia.
Lakini swali ni je?: nini hasa kinaendelea Ulaya?.
Ni vita vya Urusi na Ukraine?, Vita vya Marekani na Iran? Au ni mlundikano wa changamoto cha kiuchumi na kisiasa za muda mrefu?
Leo tunachambua mizizi ya mgogoro huu, athari zake kwa uchumi wa dunia.
Kinachoonekana mitaani ni maandamano, lakini chanzo cha hasira ni kikubwa zaidi ya tukio moja.
Wananchi wanakabiliwa na gharama kubwa za maisha, wakati baadhi yao wakiona kuwa mishahara yao haiongezeki kwa kasi inayolingana na bei za bidhaa na huduma.
Vijana wanahangaika kupata makazi yanayomudu kipato chao. Wafanyakazi wanataka mishahara bora, huku wanafunzi na makundi mengine wakitaka huduma bora za umma.
Wakati huo huo baadhi ya serikali barani Ulaya zinakabiliwa na changamoto ya kusimamia bajeti, deni kubwala taifa na gharama za huduma za kijamii.
Kwa hiyo, tatizo si kwamba Ulaya imekosa utajiri. Tatizo ni jinsi hali ya uchumi inavyoathiri maisha ya watu wa kawaida, na namna wanavyoona hatua za serikali zao.Ni muhimu pia kutofautisha maandamano ya amani na vitendo vya uharibifu vinavyofanywa na baadhi ya watu. Si kila mwandamanaji anashiriki ghasia.Sasa tuangalie upande wa kimataifa.
Kwanza, vita vya Urusi na Ukraine vilivyoanza mwaka 2022 vilitikisa soko la nishati la Ulaya. Nchi nyingi zililazimika kutafuta vyanzo vingine vya gesi na mafuta, jambo lililoongeza changamoto za gharama na usalama wa nishati.
Pili, mgogoro wa Marekani na Iran mwaka 2026 umeongeza msukosuko mpya katika soko la mafuta na gesi.
Lakini je? Kwa nini hili ni suala muhimu?
Mafuta yanapopanda bei, gharama za kusafirisha bidhaa huongezeka. Gharama za uzalishaji zinaweza kupanda, na baadaye athari hizo kufika kwa walaji kupitia bei za bidhaa na huduma.Tathmini ya ripoti ya Tume ya Ulaya ya Mei 2026 ilikadiria kuwa ukuaji wa uchumi wa Umoja wa Ulaya ungepungua kutoka asilimia 1.5 mwaka 2025 hadi asilimia 1.1 mwaka 2026, huku mfumuko wa bei ukitarajiwa kufikia asilimia 3.1. Hizi ni takwimu za utabiri, na si matokeo ya mwisho ya mwaka.
Hivyo, vita si maelezo pekee ya maandamano, lakini vinaweza kuongeza shinikizo kwenye uchumi ambao tayari una matatizo yake.Hapa ndipo kiini cha kisiasa kinapoanzia.
Wananchi wanaweza kuelewa kwamba vita vya nje vimepandisha bei za mafuta. Lakini bado wana maswali kwa viongozi wao.
Kwa nini maisha yanakuwa ghali? Kwa nini huduma za umma zinakabiliwa na changamoto? Kwa nini vijana wanapata ugumu wa kujitegemea? Na kwa nini wananchi wanahisi wanabeba mzigo mkubwa wa matatizo ya kiuchumi?
Kwa upande mwingine, serikali nazo zinakabiliwa na ukweli mgumu: zinahitaji fedha kwa ajili ya huduma za umma, miundombinu, usalama na kulipa gharama za deni.

Recommended