Skip to playerSkip to main content
  • 2 days ago
Vita vya Yemen vimeendelea kuwa chanzo cha mateso makubwa kwa wananchi, wa nchi hiyo, huku mapigano yakitishia kuongeza zaidi janga la kibinadamu nchi humo.
Hivi karibuni, shambulizi la makombora katika kambi ya mafunzo ya vikosi vya serikali ya Yemen, mkoa wa Shabwa, liliripotiwa kusababisha vifo vya watu wasiopungua 53 na kujeruhi zaidi ya 200. Idadi ya vifo iliripotiwa baadaye kuongezeka, ikionyesha ukubwa wa madhara ya mapigano hayo.
Lakini swali ni je?: kwa nini vita hivi vinaendelea, na nini hasa kiini cha mgogoro kati ya Saudi Arabia na kundi la Wahouthi?
Kiini cha tatizo ni mapambano ya madaraka nchini Yemen, yanayochochewa zaidi na ushindani wa ushawishi kati ya Saudi Arabia na Iran.
Saudi Arabia imekuwa ikiunga mkono serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa, kwa lengo la kuimarisha mamlaka yake, kulinda mipaka yake na kuzuia mashambulizi yanayoweza kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Recommended