Katibu Mkuu wa chama tawala CCM, Abdulrahman Kinana amejiuzulu kufuatia tetesi za muda mrefu kwamba alikuwa akifanya kazi katika mazingira magumu. Amekabidhi barua ya kuachia madaraka kwa Rais Magufuli.
Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa, John Magufuli aridhia ombi la kung'atuka kwa aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Rais Magufuli ametangaza kuridhia ombi hilo katika kikao cha wajumbe wa NEC, kinachofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Usipitwe na Matukio Muhimu kila siku na taarifa za Habari Mubashara yaani Live kila siku kwenye Channel hii. Subscribe sasa na bofya alama ya kengere inayotokea baada ya Subscribe. Fungua Link hii .
Be the first to comment