Sakata la Kutekwa Mo Dewji, Manara Akamatwa na Polisi

  • 6 years ago
Subscribes:
Msemaji wa Simba, Haji Manara anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Mahojiano Zaidi.

Manara anashililiwa katika kituo cha Polisi cha Mburahati jijini Dar es Salaam ambako aliitwa kwa mahojiano.

Manara alikamatwa jana jioni na kuachiwa kabla ya leo asubuhi Oktoba 12, 2018 kukamatwa tena na polisi.
Imeelezwa inahusiana na kutoa taarifa za Mo Dewji ambaye ametekwa Kwa Siku Ya Pili Sasa na upande mwingine umesema ni sehemu tu ya kazi za Polisi.


Akithibitisha kukamatwa kwa Manara, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Manara anashikiliwa kutokana na kusambaza taarifa za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kutumwa na familia, jambo ambalo si kweli.
Dewji ambaye miaka mitatu iliyopita jarida la Forbes lilimtaja kuwa tajiri namba moja Afrika kwa vijana walio chini ya miaka 40 alitekwa na Wazungu wawili waliomvizia alipokuwa akishuka kwenye gari lake ili aingie kwenye mazoezi kwenye gym ya Hoteli ya Colosseum.
Taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo anayekadiriwa kuwa na utajiri wa Sh3.5 trilioni zilianza kusambaa Alhamisi saa 1:00 asubuhi katika mitandao ya kijamii, kabla ya polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam kuthibitisha saa mbili asubuhi.
Mapema jana Manara alinukuliwa akisema taarifa ya Mo kupata matatizo imemshtua kila mmoja na kwamba bado wanaliachia jeshi la polisi kufanya kazi ya kumpata mwekezaji wao.
Subscribes: