Shambulizi La Kigaidi Lamu: Watu 6 Wafariki

  • 2 years ago
Watu 6 Wameuwawa Asubuhi Ya Kuamkia Leo Kwa Kile Polisi Wametaja Kama Shambulizi La Kigaidi. Kulingana Na Vitengo Vya Usalama, Watu Wanaoshukiwa Kuwa Magaidi Walivamia Kijiji Cha Widhu, Majembeni Kaunti Ya Lamu, Na Kutekeleza Mauaji Huku Wakiteketeza Makaazi Ya Wakaazi. Mtu Mmoja Alipigwa Risasi, Mwingine Akauwawa Kwa Kukatwa Huku Wengine Wanne Wakiteketezwa Kwenye Vyumba Vyao. Akithibitisha Kisa Hicho, Kamishena Wa Kaunti Ya Lamu Irungu Macharia Amesema Msako Kuhusu Washukiwa Hao Umeanzishwa. Polisi Wamesema Tukio Hilo Limejiri Baada Ya Washukiwa Kuonekana Msitun Boni.

Recommended