YANGA SC 1-0 COASTAL UNION; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 19/09/2018)

  • 6 years ago
Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ay Yanga imeendelea kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Coastal Union bao 1-0.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 1:00 jioni ulikuwa na mvuto wa aina yake kutokana na viwango bora vilivyooneshwa na timu zote mbili, Yanga ikiwa na nguvu zaidi kipindi cha kwanza, huku Coastal Union wakitawala zaidi kipindi cha pili.

Bao la Yanga kwenye mchezo huo limepachikwa kimiani na mshambuliaji wake Heritier Makambo dakika ya 12 ya mchezo akiitumia vyema pasi ya Ibrahim Ajib, bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo.

Hata hivyo dakika ya 35 ya mchezo, Makambo aliingia nyavuni tena lakini mwamuzi akaamua kuwa siyo bao kutokana na Papy Tshishimbi ambaye ndiye aliyetoa pasi ya mwisho, kuwa kwenye eneo la kuotea.

Baada ya mchezo huo Azam TV imezungumza na Ibrahim Ajib ambaye ameelezea siri ya kiwango chake kuwa juu kwa siku za karibuni kuwa ni kufuata maelekezo ya mwalimu na kumtegemea Mungu, huku akiwataka mashabiki wa Yanga kujiandaa kuchukua kombe la ligi hiyo msimu huu.

Naye kiungo wa Coastal Union Mtenje Albano ameelezea sababu za timu yake kuelemewa zaidi kipindi cha kwanza kabla ya kuingia kwake dimbani.

Recommended