HARMONIZE Alivyomwaga Machozi Kisa DIAMOND - KUSINIGHT

  • 6 years ago
HARMONIZE Alivyomwaga Machozi Kisa DIAMOND - KUSINIGHT

STAA wa Bongo, Nasu Abdul ‘ Diamond Platinumz’ amefanya sapraizi ya aina yake na kuwashangaza mashabiki zake baada ya kuibuka kwenye shoo ya Usiku wa Kusini ‘KusiNight’ iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakiem.

Shoo iliyokuwa maalum kwa Harmonize, Diamond alishindwa kujizuia na kutoka huko alikokuwa usiku wa manane kisha kuvamia stage ya Dar Live na kugonga nyimbo mbili ikiwemo mpya aliyoshirikishwa na Harmonize, Kwangwaru huku mashabiki wakishindwa kuelewa Mond kaibukia wapi.

Baada ya Diamond kuvamia jukwaa, mashabiki walilipuka kwa shangwe, akaungana na Harmonize huku shoo ikianza upya, mashabiki wakipagwa, na burudani ikanoga kwani hakuna aliyefahamu endapo Mondi angefanya Sapraizi kama hiyo. Mmanyema na Mmakonde wakaliamsha dude, haikua kazi ya kitototo.

Ikumbukwe kwamba, Jukwaa la Dar Live ndilo lilianza kuonyesha njia ya mafanikio ya muziki wa Harmonize mwaka 2015 baada ya kupewa nafasi ya na Diamond ya kuimba kwenye jukwaa hilo, ndipo kipaji chake kilionekana na Mond akamchuku.

Hivyo usiku wa kuamkia leo ilikuwa ni kumbukumbu muhimu kwa wawili hao kukutana tena jukwaa moja lililowakutanisha siku ya kwanza. Mbali na hivyo, iliuwa siku muhimu kwa kumbukumbu ya kipekee ya Harmonize alivyoanza safari yake ya muziki.

Install GlobalPublishersApp Android: iOS: Subscribe FACEBOOK: ...

TWITTER: Visit , Subscribe Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…

WEBSITE: FACEBOOK: ... TWITTER: INSTAGRAM: ..

Recommended