Serikali Yawarai Vijana Kuepukana Na Siasa Chafu Za 2022

  • 3 years ago
Serikali imewarai vijana katika ukanda wa Pwani kususia kutumika vibaya na wanasiasa hasa taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao. Msemaji wa serikali Cyrus Oguna ametaja kuwa tayari vijana 500 kutoka eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa wamebadilisha tabia zao kutokana na visa vya uhalifu na jitihada hizo katu hazipaswi kuangamizwa na siasa. Hata hivyo serikali imeradidi kuwa ipo na mipango kabambe yakuunda sera za kuwafaa vijana nchini.