Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Sita
  • 5 years ago
Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Sita
Mwenyezi Mungu anasema, “Namna ambavyo Mungu anawatendea watu wanaomkufuru au hata wanaompinga, au hata wale wanaomkashifu—watu wanaomshambulia kimakusudi, kumkashifu, na kumlaani—hajifanyi kwamba kila kitu kiko sawa. Anao mwelekeo wazi kwa hawa. Anawadharau watu hawa, na moyoni Mwake anawashutumu. Anatangaza waziwazi hata matokeo kwa ajili yao, ili watu waweze kujua kwamba Anao mwelekeo wazi kwao wanaomkufuru Yeye, na ili wajue namna atakavyoamua matokeo yao. Hata hivyo, baada ya Mungu kusema mambo haya, watu bado wangeona kwa nadra ukweli wa namna ambavyo Mungu angeshughulikia watu hao, na wasingeelewa kanuni zinazotawala matokeo ya Mungu, hukumu Yake kwao. Hiyo ni kusema, wanadamu hawawezi kuuona mwelekeo na mbinu fulani za Mungu katika kuwashughulikia. Hali hii inahusu kanuni za Mungu za kufanya mambo. Mungu hutumia ujio wa hoja katika kushughulikia tabia yenye uovu ya baadhi ya watu. Yaani, Hatangazi dhambi yao na haamui matokeo yao, lakini Anatumia moja kwa moja ujio wa hoja ili kuwaruhusu kuadhibiwa, wao kupata adhabu wanayostahili. Wakati hoja hizi zinapofanyika, ni miili ya watu inayoteseka kwa adhabu; hili ni jambo ambalo linaweza kuonekana kwa macho ya binadamu. Wakati wa kushughulikia tabia ya uovu kwa baadhi ya watu, Mungu huwalaani tu kwa matamshi, lakini wakati uo huo, ghadhabu ya Mungu huwapata, na adhabu wanayopokea inaweza kuwa jambo ambalo watu hawalioni, lakini aina hii ya matokeo inaweza kuwa hata mbaya zaidi kuliko matokeo ambayo watu wanaweza kuona ya kuadhibiwa au kuuawa.”

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Injili ya Kushuka kwa Ufalme: https://sw.kingdomsalvation.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu: https://sw.godfootsteps.org/
Recommended