JOSEPH SELASINI: KUNA HOFU KUBWA KUWA WANAJESHI WA RWANDA WANALINDA SEHEMU NYETI ZA NCHI YETU
  • 6 years ago
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini amesema Majeshi la Ulinzi ya Tanzania yanafanya kazi nzuri na yanaheshimika katika nchi za Afrika ila yanaharibiwa na wanasiasa,

Mbunge huyo amesema kwa kutumika huko kisiasa, majeshi, hasa jeshi la Polisi linapoteza umakini wake hali inayopelekea kutokea matukio mbalimbali ya kigaidi ambayo yameshindwa kudhibitiwa na jeshi hilo,

Akitolea mfano wa matukio ya Kibiti na ya watu kutekwa na kupigwa risasi, Selasini alisema jeshi la Polisi linahitaji kitengo makini cha upelelezi ili kuwang'amua wahusika wa matukio hayo,

Akichangia kwenye bajeti ya Wizara ya Ulinzi, Bungeni Dodoma, Selasini alisema kuna hofu kubwa kuwa baadhi ya maeneo nyeti hapa nchini inasemekana yanalindwa na askari kutoka Rwanda,

"Hofu hizo ni lazima ziondolewe kwani inawezekana watu hao wakahusishwa na watu wasiojulikana. Hivyo kuna ulazima kitengo cha upelelezi cha Jeshi la Polisi kikaimarishwa ili kiwe na nguvu ya kufanya uchunguzi kwenye maeneo hayo yenye hofu," alisema Selasini

Mbunge huyo alisema Jeshi la Polisi la Tanzania lina uwezo na haoni kama kuna umuhimu wa kuleta wanajeshi kutoka nchi jirani.
Recommended